Isaiah 28:14-15


14 aKwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau
mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.
15 bNinyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,
tumefanya mapatano na kuzimu.
Wakati pigo lifurikalo litakapopita,
haliwezi kutugusa sisi,
kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu
na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”
Copyright information for SwhNEN